Akiwa na umri wa miaka 26 pekee, Kylian Mbappé amefanikiwa kuweka mchango wa mabao 500 kutoka miguuni na kichwani kwake ikimfanya kuweka alama ya kipekee katika umri huo. Hii inajumuisha mabao 358 na asisti 142 kwa klabu na timu ya taifa. Amefikia alama hii katika mechi ya mtoano wa awali raundi ya 32 dhidi ya Manchester City, ambapo ameifungia bao la kwanza la Real Madrid.
Kylian Mbappé amejidhihirisha kama mchezaji wa kipekee katika mechi kubwa, akitoa mchango muhimu kwa klabu na timu ya taifa.
Kombe la Dunia la FIFA 2018 Mbappé alionyesha uwezo wake akiwa na umri wa miaka 19, akifunga mabao manne na kusaidia Ufaransa kutwaa ubingwa. Akiwa mchezaji mdogo zaidi wa Ufaransa kufunga kwenye Kombe la Dunia na kijana wa pili baada ya Pelé kufunga kwenye fainali ya Kombe la Dunia.
Ligi ya Mabingwa Ulaya Mbappé amefunga mabao 52 katika mechi 82 za Ligi ya Mabingwa, akishika nafasi ya nane katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo.