Matumizi ya Internet kuchochea mapinduzi ya kidijitali Tanzania

Sekta ya kidijitali nchini Tanzania inashuhudia mabadiliko makubwa, yanayoongozwa na ongezeko kubwa la upatikanaji wa intaneti, jambo linalo weka muelekeo wa kuleta manufaa makubwa kwa uchumi wa taifa.

Ripoti ya hivi karibuni inaonyesha kuwa watumiaji wapya wa intaneti takriban milioni saba wameongezeka ndani ya miezi mitatu pekee.

Ukuaji huu unakwenda sambamba na dhamira ya Tanzania ya kukuza uchumi wa kidijitali, kupitia Mwongozo wa Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa mwaka 2024-2034, ambao ulizinduliwa mwezi Julai 2024.

Mkakati huu unalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuimarisha miundombinu ya kidijitali, kuimarisha upatikanaji wa mtandao, na maendeleo ya kiteknolojia.Lengo kuu ni kupanua huduma za mtandao wa kasi na kuboresha ubora wa mitandao ili kuhakikisha kwamba Watanzania wote, hususan waishio maeneo ya vijijini na yasiyo na huduma za kutosha, wanapata intaneti ya uhakika.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), idadi ya usajili wa intaneti imeongezeka kutoka milioni 41.4 katika robo ya tatu ya mwaka 2024 hadi kufikia milioni 48 mwishoni mwa mwaka huo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *