Marcus Jordan adakwa na dawa za kulevya.

Mtoto wa aliyekuwa gwiji wa mpira wa kikapu duniani, Michael Jordan amekamatwa jijiji Florida kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa huku akikutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine. Polisi walifanikiwa kumkamata baada ya kugundua gari lake aina ya Lamborghini limekwama kwenye reli za treni.

Taarifa zinadai Marcus aligoma kushirikiana na polisi hali iliyopelekea kufanyiwa upekuzi kwenye gari lake ambapo zilikutwa dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Marcus kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani huku rekodi ikionyesha sio mara ya kwanza kwa Marcus kukutwa na makosa na matumizi ya madawa haramu kwani amewahi kufanya hivyo mwaka 2012.

Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka familia ya Jordan huku wengi wakisubiri kusikiliza maamuzi ya sheria juu yake.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *