Man City na Arsenal kuchuana kwa Nypan.

Tetesi za usajili barani Ulaya zinaendelea na awamu hii vigogo wawili nchini Uingereza kuchuana kupata saini ya kiungo chipukizi Sverre Nypan kutoka klabu ya Rosenborg ya nchini Norway.

Awali ilisemekana kuwa Nypan anakwenda uwanja wa mazoezi wa Manchester City kukutana na Kocha Pep Guardiola kuangalia uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo ambapo Manchester City wana mpango wa kumnunua kisha kumpeleka katika Klabu ya Girona ya nchini Hispania kwa mkopo.

Zimeibuka taarifa mpya kwamba Arsenal wamefikia makubaliano mazuri na klabu yake ya Rosenborg pamoja na mchezaji husika huku wakimhakikishia nafasi ya kucheza katika timu ya ushindani.

Sverre Nypan anatarajia kufanya maamuzi kuhusiana na Klabu atayojiunga nayo Januari hii huku Klabu ya Manchester United na Real Madrid zikihitaji huduma yake pia.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *