Mahakama yamsamehe Trump mashitaka yake.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amepewa msamaha wa moja kwa moja dhidi ya kesi ya kughushi nyaraka za biashara kuficha malipo kwa msanii Stormy Daniels.

Hapo awali Trump alikuwa ameshtakiwa kwa makosa 34 ya kughushi nyaraka akidaiwa kuficha malipo ya dola 130,000 kwa Stormy Daniels ili kuficha madai ya uhusiano wao wa kimapenzi ambapo inasemekana kuwa kesi hii ilihusika na jitihada za kulinda kampeni yake ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Aidha Jaji mkuu wa kesi hiyo Juan Merchan amesema kuwa msamaha huo umelenga kuepusha kuathiri majukumu ya urais japo hukumu hiyo haiwezi kuondolewa kwenye rekodi yake.

Hukumu hii inamfanya Trump kuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhukumiwa kwa makosa ya jinai kisha kurejea ikulu. Trump anatarajiwa kuapishwa kama Rais mpya wa Marekani siku chache zijazo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *