Mahakama imewezesha magereza kumi usikilizwaji wa kesi kwa njia ya mtandao

Mahakama ya Tanzania imekabidhi makasha 10 ya kisasa ya Mahakama Mtandao kwa Jeshi la Magereza, yatakayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya mtandao ili kusaidia utoaji haki kwa wakati, kupunguza msongamano wa wahalifu magerezani pamoja na kupunguza gharama za usafirishaji wa wafungwa na mahabusu kwenda mahakamani kusikiliza mashauri yao.

Makabidhiano hayo yamefanywa kati ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof. Elisante Ole Gabriel, na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP Jeremiah Y. Katungu, na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, katika Gereza la Isanga -Dodoma, tarehe 21 Machi 2025.

Akizungumza baada ya kuzindua na kushuhudia makabidhiano hayo, Waziri Bashungwa amesema makasha hayo yatakayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya mtandao ambao ni daraja linalounganisha mahabusu na haki na yatasaidia kupunguza gharama za usafiri pamoja na kuahirishwa kwa kesi kutokana na mahabusu kushindwa kufikishwa mahakamani.

Mahakama Mtandao inarahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama, kuokoa gharama za uendeshaji, kupunguza msongamano wa wananchi mahakamani, kuwezesha mawakili kupata rejea za hukumu na nyaraka mbalimbali kwa urahisi, na pia kuwabaini mawakili vishoka ambao wamekuwa wakiharibu mwenendo wa kesi mbalimbali,” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema usikilizaji wa mashauri kwa njia ya mtandao ni mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kusaidia taasisi za haki jinai na kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *