Mtangazaji wa Clouds FM, Alex Luambano ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA) na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Mohamed Saleh Mohamed.
Hatua hiyo imekuja baada ya Luambano hapo awali kushindwa kwenye uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti cha chama hicho dhidi ya Mohamed Saleh Mohamed. Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho Mwenyekiti ana uwezo wakuchagua Makamu wake iwapo atashinda hivyo Mohamed Saleh Mohamed aliamua kumchagua Alex Luambano kama Makamu wake katika chama hicho.
Katika uchaguzi huo wa nafasi ya Uenyekiti Mohamed Saleh Mohamed alipata kura 28 huku Alex Luambano akipata kura 16 kati ya 48 zilizopigwa huku kura 2 zikiharibika.