Ligi ya mabingwa barani Ulaya imezidi kushangaza wengi baada ya klabu ya Liverpool iliyokuwa inapewa nafasi kubwa yakubeba taji hilo kujikuta inaaga mashindano hayo mbele ya Psg katika uwanja wa Anfield.

Liverpool waliokuwa wanapewa nafasi kubwa yakushinda wamejikuta wanafungwa mechi hiyo iliyolazimu kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Psg aliibuka kidedea kwa ushindi wa 4-1.

Michezo mingine imeshuhudia kuona Bayern Munich akifuzu hatua ya robo fainali baada ya kumtoa Bayer Leverkusen huku Inter Milan wakifuzu baada ya kumtoa Feyenoord.

Macho ya wapenzi wa soka yatahamia kwenye mtanange mwingine leo ambapo Real Madrid atamenyana na hasimu wake Atletico Madrid kwenye mchezo wa dabi utakaofanyika katika dimba la Wanda Metropolitano ambapo mshindi atafuzu hatua ya robo fainali.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *