Ligi Kuu NBC Tanzania kurejea mapema Februari

BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya tarehe ya kurejea kwa michezo ya Ligi Kuu NBC ambayo hapo awali ilipangwa kuendelea Machi 1. 2015 baada ya kutamatika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi na fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN)

Michezo ya ligi Kuu ya NBC sasa Itarejea katika Juma la kwanza la Februari 2025 huku ikitarajiwa kuanza kwa michezo ya viporo kabla ya kuendelea na ratiba ya mechi za mzunguko wa 17,huku Tarehe rasmi pamoja na ratiba iliyofanyiwa maboresho, kutangazwa hivi karibuni.

Mabadiriko hayo yamekuja baada ya Shirikisho la Soka afrika Caf kusogeza mbele fainali za CHAN kutoka Februari 1, 2025 hadi Agosti, 2025 ivyo kutoa nafasi kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea na michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo ilisimama kupisha fainali hizo.

Bodi ya Ligi imetoa wito kwa klabu zote kuhakikisha zinaongeza nguvu katika maandalizi ya timu kiufundi pamoja na masuala mengine haswa yahusuyo miundombinu ya viwanja, na vitakaguliwa kabla ya kurejea kwa Ligi.

Viwanja vitakavyoonekana kukosa sifa vitaondolewa katika orodha na klabu mwenyeji hatalazimika kuteua uwanja mwingine miongoni mwa vilivyothibitishwa kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *