Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaachia Masheikh 51 wanaoshikiliwa katika magereza tofauti tofauti kwa takriban miaka 10 sasa bila kufikishwa mahakamani ikiwa ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
LHRC inadai kuwa kitendo cha Jamhuri kuwafunga miaka yote hiyo bila kuwafikisha mahakamani kinaashiria kuwa hakuna ushahidi wa kutosha unoweza kuwatia hatiani watuhumiwa hivyo inaomba Jamhuri iwaachie haraka kama hakuna ushahidi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Wakili Fulgence Massawe ametoa rai kwa DPP (Mwendesha mashtaka wa Serikali) kusimamia haki kwa kila anayekabiliwa na mashtaka na kutotumia na kutotumia mamlaka aliyo nayo vibaya kama hana ushahidi.