Baada ya mzozano baina ya Rais Donald Trump na Rais Vlodymr Zelensky wa Ukraine, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amewapigia simu viongozi hao wawili kuwasihi wamalize tofauti zao na kuendeleza maongezi kuhusiana na ajenda husika.
Aidha Rais wa Marekani Donald Trump amesema anahitaji yeye ana Marekani kwa ujumla kuombwa radhi hadharani kwa kilichotokea.
Mzozano baina ya wawili hao uliotokea ikulu ya nchini Marekani ulishuhudia kumuona Rais Vlodymr Zelensky wa Ukraine akiondoka bila maridhiano baina ya pande hizo kufanyika kwa kile kilichosemekana kutofautiana kauli na Rais Trump.
Licha ya mzozano huo Rais wa Ukraine alidai hajaona alipokosea hivyo haoni haja ya kuomba msamaha. Rais Trump amedai bila msamaha wa hadharani hakutakuwa na maridhiano wala uhusiano baina ya nchi hizo mbili ambazo zilikuwa zina uhusiano mzuri hapo awali.