Kinda wa Arsenal kukipiga timu ya taifa Uingereza

Beki wa kikosi cha Arsenal MylesLewis-Skelly ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa cha England chini ya kocha mpya Thomas Tuchel kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Nyota wa Arsenal, Declan Rice, naye amejumuishwa kwenye kikosi kitakachovaana na Albania na Latvia katika Uwanja wa Wembley, Ijumaa, Machi 21 na Jumatatu, Machi 24.Lewis-Skelly ameonyesha kiwango bora msimu huu, akitamba kwenye kikosi cha Arsenal baada ya kupanda kutoka akademi ya Hale End.

Mpaka sasa, amecheza mechi 13 kwenye Ligi Kuu ya England na michezo sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2024/25, jambo lililomvutia Tuchel kumjumuisha katika kikosi cha Three Lions.Katika ngazi ya kimataifa, Myles amepitia hatua zote za maendeleo kwenye timu za vijana za England, akiichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 16, 17, 18 па 19.

Kwa upande mwingine, Declan Rice ana uzoefu mkubwa wa kimataifa akiwa na mechi 62 kwenye jezi ya England, na wote wawili wanatarajia kufanya kazi chini ya Tuchel kwa mara ya kwanza katika kikosi cha taifa.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *