Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Halmashauri Kuu CCM Taifa, imefanya kikao chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo katika kikao hicho Halamshauri imepitisha kauli mbiu mpya kwaajili ya kampeni za uchaguzi wa 2025.
Kauli mbiu hiyo inasema “KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE”
CCM wamesema kauli mbiu hiyo inaonyesha dhamira ya chama ya kuendeleza juhudi za ujenzi wa taifa lenye maendeleo jumuishi, mshikamano wa kitaifa na ustawi wa watu wenye kujali utu.