Mkuu wa vikosi vya ulinzi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametishia kushambulia na kuuteka mji wa Bunia ulio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kupitia mtandao wa X, Jenerali Muhozi alisema “Bunia hivi karibuni itakuwa mikononi mwa UPDF”.
Aliendelea kwa kusema “Watu wangu Bahima wanashambuliwa. Hiyo ni hali ya hatari sana kwa wale wanaowashambulia watu wangu. Hakuna mtu katika dunia hii anayeweza kuwaua watu wangu na kufikiri hatateseka kwa ajili yake,”.
Aidha Waziri Mkuu wa Congo Judith Suminwa amesema kuwa Serikali yake haina maoni ya kutoa juu ya kauli za Jenerali Muhoozi.