Serikali ya Japan imesema inatambua umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam kama kiungo muhimu cha biashara kati ya Japan na Ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika.
Hayo yamesemwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Balozi Yasushi Misawa alipoongoza ujumbe wa Wawekezaji kutoka Sekta ya Umma na Binafsi wa Japan, walipokutana na kuzungumza na uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa majadiliano ya kibiashara na ziara ya mafunzo kuhusu tozo za kiforodha katika Bandari ya Dar es Salaam.
Awali akizungumza wakati akimkaribisha Balozi na ujumbe wake, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. George Fasha, amesema ili kurahisisha mchakato wa Uchukuzi wa shehena, TPA imefungua ofisi katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Burundi.