Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo ameipongeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kusajili kidijitali.
Akizungumza hayo wakati akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Dimani, Zanzibar. Waziri Jafo amefurahishwa kuona taasisi mbalimbali za usjaili zinavyofanya usajili kielektroniki na kupunguza foleni na usumbufu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
“Usajili w kidijitali unakwenda sambamba na kaulimbiu ya maonyesho haya ambayo ni biashara mtandao kwa maendeleo ya biashara na uwekezaji, hongereni sana.” Alisema.
NIDA imeweka utaratibu wa kujisajili kidijitali pia mwombaji wa kitambulisho anaweza kufahamu namba yake ya utambulisho wa taifa (NIN) na mahali kilipo kitambulisho chake.