IMF wahimiza uwekezaji wa dola bilioni 25 kila mwaka sekta ya nishati Afrika

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema kuwa uwekezaji wa kiasi cha dola bilioni 25 kila mwaka katika sekta ya nishati mbadala barani Afrika unaweza kuongeza uzalishaji wa umeme kwa asilimia 20.Kwa kuwa nishati mbadala ni kiini cha ukuaji wa kiuchumi, kupunguza umasikini, na ustawi endelevu barani Afrika, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bw. Bo Li

alibainisha kuwa uwekezaji huo pia unaweza kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) kwa asilimia 0.8 kila mwaka katika muongo mmoja ujao.Akizungumza katika Mkutano wa Nishati wa Mission 300 Africa uliofanyika Dar es Salaam, Bo Li alieleza jukumu muhimu la nishati mbadala katika kubadilisha bara hilo.

Aliwaambia zaidi ya wajumbe 1,000 katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kwamba serikali za Afrika lazima ziongoze katika kuunda mazingira yanayovutia uwekezaji endelevu wa kifedha.“Kudumisha utawala bora na uwazi, kutekeleza kanuni madhubuti, na kufanya mageuzi ni hatua muhimu za kuongeza mtiririko wa fedha endelevu,” alisema, akitaja zana kama makubaliano ya ununuzi wa nishati, viwango vya bei ya kununua umeme (feed-in tariffs), na malengo ya nishati mbadala kama njia za kuwahakikishia wawekezaji faida za baadaye.

Mfuko wa IMF wa Ustahimilivu na Uendelevu (RST) umeibuka kama mpango muhimu wa kusaidia nchi za Afrika kushughulikia changamoto za nishati na mabadiliko ya tabianchi.“Mfuko wetu wa RST wenye dola bilioni 48 unasaidia mataifa yenye changamoto kujenga ustahimilivu,” alisema Bo Li. “Hadi sasa, tumekubali kutoa dola bilioni 10 kwa nchi 21, zaidi ya nusu zikiwa ni za Afrika.”

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *