Idadi ya vifo huko Goma inaendelea kuongezeka, huku miili ikiendelea kuonekana ikielea katika Ziwa Kivu na mingine bado ikikusanywa.

Bounena Sidi Mohamed, naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), alisema kuwa angalau miili 2,000 tayari imezikwa na jamii, huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema Jumatano kuwa miili 900 bado iko katika vyumba vya kuhifadhi maiti huko Goma.

Miili mingi iliyooza bado ipo katika maeneo fulani, hasa karibu na uwanja wa ndege wa Goma na gereza.Hali ya kibinadamu katika jiji la Goma ni ya kutisha baada ya mapigano ya siku nne wiki iliyopita.”Taasisi za afya zimepata ugumu wa kuhakikisha viwango vya usafi vinavyohitajika kudhibiti maambukizi, na baadhi ya hospitali zimeshuhudia wagonjwa wakifariki kutokana na matatizo ya upumuaji. Nyingine zimesitisha shughuli zao kwa sababu haziwezi kutumia vifaa vya uangalizi wa wagonjwa, kuendesha vyumba vya upasuaji, au kuua vijidudu kwenye vifaa. Katika hali nyingine, kukatika kwa umeme kumeathiri uhifadhi wa dawa na vyumba vya kuhifadhi maiti,” limesema Shirika la Msalaba Mwekundu la Kimataifa (ICRC).

Usumbufu wa upatikanaji wa maji safi ya kunywa umewalazimu watu kutumia maji yasiyochujwa moja kwa moja kutoka ziwani, hali inayowaweka katika hatari ya magonjwa yanayosababishwa na maji machafu kama kipindupindu, ambacho ni tatizo sugu katika eneo hilo.

Kuna changamoto nyingi zinazowakabili wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na matatizo ya afya na upungufu wa mifuko ya kuhifadhia maiti. Kwa sasa, mifuko 500 pekee ndiyo inapatikana, ikiwa ni pamoja na 100 kwa watoto na 400 kwa watu wazima,alisema Bi Mohamed.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *