Henry atupa karata yake kwa Arsenal dhidi ya Madrid.

Gwiji wa soka na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry anaamini kuwa timu yake ya zamani ya Arsenal ina uwezo wa kuitoa Real Madrid kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA) licha ya kwamba hawapewi nafasi.

Henry amedai kuwa Arsenal hii inauwezo wakupambana na Real Madrid na wanachotakiwa kufanya ni kujiamini tu kuwa wanaweza na kufanya kweli.

Katika michuano hiyo timu hizo zimewahi kutana mara mbili ambapo Arsenal alifanikiwa kufuzu katika uwanja wa ugenini kwa goli pekee la Thierry Henry liloinyamazisha Real Madrid katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu na kuwawezesha Arsenal kufuzu fainali.

Real Madrid wanapewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo kwa kuwa na historia inayowabeba linapokuja swala la michuano hiyo huku Arsenal wakijaribu kuweka historia mpya kwa kubeba taji hilo ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *