Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameachana na mke wake Cristina Serra ambaye amedumu naye kwa miaka 30 wakiwa kwenye uchumba na ndoa.
Taarifa zinadai kuwa wawili hao hawapo pamoja kwa miaka mitano tangu Cristina alipoamua kuondoka Uingereza na kutimkia nchini Hispania akiwa na mtoto wao Valentina (17) huku akimuacha Pep Uingereza.
Wawili hao walikutana rasmi mwaka 1994, walifanikiwa kufunga ndoa 2014 na wana watoto watatu ambao ni Maria (24), Marius (22) na Valentina (17).
Hata hivyo taarifa zinadai mwanzo hakukuwa na taarifa halali ya wawili hao kuachana kwani walikuwa wakionekana pamoja Hispania na Uingereza kwa vipindi tofauti.