Bundi la majeruhi limeendelea kuitesa Arsenal na sasa mshambuliaji wake Gabriel Jesus anatarajiwa kukosekana kwa kipindi kirefu kutokana na kuchanika mishipa ya goti.

Hilo limethibitishwa na kocha Mikel Arteta ambaye ameongeza kuwa Arsenal itaingia sokoni Januari hii kujaribu kupata mrithi wa mshambuliaji huyo kwa njia ya mkopo au manunuzi ya jumla.

Wakati hayo yakiendelea klabu ya Arsenal inatazamiwa kukamilisha usajili wa kiungo wa Real Sociedad, Martin Zubimendi ambaye atawasili klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu kuanza kutumika msimu ujao. Vilevile Borussia Dortmund wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kushoto wa Arsenal Oleksandr Zinchenko kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua mwisho wa msimu.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *