Kuanzia mwanzo wa msimu wa 2025/26, makipa wataadhibiwa kwa kushikilia mpira kwa zaidi ya sekunde nane.
Kosa hili litaadhibiwa kwa mwamuzi kuipa timu pinzani mpira wa kona.Hii ni mabadiliko ya Sheria ya 12.2, ambayo hapo awali ilieleza kuwa mpira wa adhabu usio wa moja kwa moja ama faulo unatakiwa kutolewa baada ya sekunde sita, ingawa makipa mara chache sana waliadhibiwa kwa kushikilia mpira kwa muda mrefu zaidi.
Kocha wa Liverpool, Arne Slot, ni miongoni mwa wale waliokosoa waamuzi wa Ligi Kuu kwa kupuuza sheria hii, hivyo huenda akapokea mabadiliko haya kwa mikono miwili.
Waamuzi pia watatumia msaada wa kihesabia muda kuona mahesabu ya sekunde hizo wakati sheria hii itakapoanza kutumika, wakihesabu sekunde tano za mwisho kabla ya kipa kulazimika kuachia mpira.
Marekebisho haya yanamaanisha kuwa endapo kipa atashikilia mpira kwa zaidi ya sekunde nane (na mwamuzi akitumia hesabu ya sekunde tano za mwisho), basi mwamuzi ataipa timu pinzani mpira wa kona badala ya mpira wa adhabu ya faulo kwa sekunde sita kama ilivyo kuwa apo awali.