Fedha ya China Yuan yashuka Thamani

Fedha ya China yaanguka kiwango cha chini kabisa cha miezi 16 siku ya Jumatatu, licha ya juhudi za benki kuu na masoko ya hisa kutuliza hofu kwa wawekezaji kuhusu ushuru mkubwa wa Marekani chini ya urais wa Donald Trump.

Yuan, ambayo inadhibitiwa kwa ukaribu, ilifikia kiwango cha 7.3301 kwa dola moja ya Marekani,ikiwa ni kiwango chake dhaifu zaidi tangu Septemba 2023. Kuanguka huko kuna husishwa na Trump kushinda uchaguzi wa Marekani, akiahidi ushuru mkubwa kwa bidhaa za China.

Kielelezo cha hisa za blue-chip, CSI 300, pia kilifanya vibaya siku ya Jumatatu, kikifikia kiwango chake cha chini zaidi tangu Septemba, kikishuka angalau asilimia 0.9kabla ya kufunga na kupungua kwa asilimia 0.2. Hii ilikuja baada ya kielelezo hicho kuripoti hasara kubwa zaidi ya kila wiki katika zaidi ya miaka miwili wiki iliyopita, ikifikia anguko la asilimia 5.

Kwa wiki mbili kabla ya Trump kuanza kipindi chake cha pili cha urais, matarajio ya ushuru mkubwa kwa bidhaa za China yameongeza kuyumba kwa masoko ya China, yakishusha viwango vya bondi za bara na kuyumbisha hisa.

Hali hii imeongeza wasiwasi kwenye soko ambalo tayari lina wasiwasi kuhusu matatizo ya kiuchumi yanayoendelea nchini humo, ambayo yamesababisha upotevu wa mitaji.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *