Exim yafanikisha ununuzi benki ya Canara.

Benki ya Exim imetangaza kufanikisha mkakati wa kununua benki ya Canara Tanzania ikiwa ni ununuzi wao wa benki ya tatu ndani ya miaka sita.

Safari yao ilianza mwaka 2016 kwa ununuzi na uboreshaji wa benki nchini Uganda, walianza kununua UBL bank mwaka 2019, FNB bank mwaka 2022 na sasa Canara bank mwaka 2024.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw. Jaffari Matundu amesema kuwa ununuzi huo ni hatua ya kimkakati ya kuongeza ukuzi wa benki yao pamoja na kuboresha sekta ya kibenki ndani na nje ya Tanzania ambayo itachangia maendeleo endelevu ya kiuchumi.

Aidha Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Bw. Shani Kimswaga amesema kuwa Benki ya Canara imekuja kuongeza mali za benki ya Exim ambapo hadi kufikia sasa zinafika shilingi Trilioni 3.1.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *