Ex wa kipa Real Madrid adai huduma ya mtoto wa nje ya ndoa

Golikipa namba moja wa klabu ya Real Madrid, Thibaut Courtois amekumbwa na madai kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Elsa Isaac, ambaye anadai kwamba kipa huyo wa Real Madrid haitoi msaada wa kutosha kwa mtoto wao wa nje ya ndoa.

Elsa, ambaye ni mbunifu wa zamani wa Versace, amesema kwamba nyumba yake yenye thamani ya pauni milioni 3 iko hatarini kupokonywa kutokana na deni kubwa la rehani.

Elsa na Courtois walihusiana kimapenzi mwaka 2014, kipindi ambacho kipa huyo alikuwa akiichezea Chelsea na walikuwa majirani.Mahusiano yao yalipelekea kupata mtoto, lakini kwa sasa Elsa anadai kuwa hana msaada wa kutosha kifedha kutoka kwa Courtois ili kumtunza mtoto huyo.

Wakati hayo yakiendelea, Courtois ameendelea na maisha yake na sasa ameoa. Anaye binti wa miezi 11 na mke wake, pamoja na watoto wengine wawili waliotokana na mahusiano yake ya awali.

Hadi sasa, Courtois hajatoa tamko lolote rasmi kuhusiana na madai haya kutoka kwa Elsa Isaac.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *