Moto umezuka uwanja wa Manchester City wa Etihad masaa machache kabla ya mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Club Brugge.
Moto huo umeanzia kuwaka kwenye sehemu za kuuzia Jezi hatua chache kutoka kwenye Jukwaa.
Aidha taratibu kadhaa zinafanyika kuzima moto huo kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kufanyika masaa machache siku ya leo.