Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mwanasiasa mkongwe nchini Dkt. Wilbroad Slaa kupelekwa Mahakamani mwezi Machi tarehe 4 wakati kesi yake ya kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii itakapotajwa.
Dkt Wilbroad Slaa ambaye amewahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na mgombea wa Urais mwaka 2010 anakabiliwa na shutuma za kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X, kinyume cha Sheria.
Hakimu wa kesi hiyo Ndg. Ushindi Swallo ametoa amri hiyo baada ya upande wa utetezi kuwasilisha ombi mahakamani wakiomba mteja wao awe anapelekwa mahakamani hapo wakati kesi yake inapotajwa.