Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amepitishwa kugombea Urais kwenye uchaguzi wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi amemteua Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake wa Urais kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Aidha Dkt. Nchimbi ataendelea kuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa sasa hadi Uchaguzi Mkuu utakapofanyika.