Dkt. Mpango azitaka taasisi za viwanda kufanya tafiti teknolojia ya nishati safi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa taasisi kama Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), TEMDO na nyingine kutafiti na kutengeneza teknolojia mbalimbali zinazotumia nishati safi na zenye gharama nafuu ili ziweze kusaidia uhamaji kwenda kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa na sekta binafsi kwa ujumla kujitolea kusaidia majiko na teknolojia rahisi kwa shule na vituo vinavyolea watoto na watu wenye mahitaji maalum.

Ametoa wito huo wakati akifungua Kongamano la Wanawake Duniani Kanda ya Magharibi linalofanyika Mkoani Kigoma.

Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa Mwaka 2024-2034 ambao unalenga kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Vilevile amesema Serikali imesaini makubaliano ya awali na wawekezaji kuhusu Ruzuku ya Sh. Bilioni 8.64 kwa ajili ya nishati safi ya kupikia, ambapo jumla ya majiko 452,455 yamepata ruzuku kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa wananchi kwa gharama nafuu.

Hali kadhalika Makamu wa Rais amewasihi wanawake kushiriki kikamilifu katika kutoa hamasa kuhusu jukumu muhimu la kujiandikisha kupiga kura, kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kushiriki kuchagua viongozi wanaowapenda. Amesema ni jukumu la kila mmoja kujenga na kudumisha umoja, amani, mshikamano na kuepuka vurugu katika mchakato wote wa uchaguzi.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *