Deni la Taifa laongezeka kufikia trilioni 100.

Deni la taifa la Tanzania limefikia Sh trilioni 97.35 kufikia Juni 30, 2024, likiwa limeongezeka kwa Sh trilioni 15.1 kutoka Sh trilioni 82.25 zilizorekodiwa katika mwaka wa fedha wa 2022/23, kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere.

Katika ripoti aliyoiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu, Alhamisi, Machi 27, 2025, Kichere alisema kuwa, licha ya ongezeko hilo kubwa, deni la serikali bado linaweza kuhimiliwa kwa kuzingatia viashiria muhimu vya uchumi.”Deni la serikali lilifikia Sh trilioni 97.35 kufikia Juni 30, 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.36 kutoka mwaka uliopita. Kati ya kiasi hiki, Sh31.95 trilioni ni deni la ndani, huku Sh trilioni 65.40 likiwa ni deni la nje,” alisema Kichere.

CAG alieleza kuwa tathmini ya uhimilivu wa deni imeonyesha kuwa nchi iko katika hali inayoelezeka, huku viwango muhimu vikionyesha kuwa mikopo inachukuliwa kwa uwiano mzuri. Deni la nje kama asilimia ya Pato la Taifa (GDP) ni 23.6, chini ya kikomo cha asilimia 40. Jumla ya deni la taifa ni asilimia 41.1 ya GDP, bado ikiwa chini ya kikomo cha asilimia 55.

Kwa mujibu wa Kichere, kiwango cha kulipia deni kwa kutumia mapato ya mauzo ya nje bado kiko ndani ya kiwango kinachoweza kudhibitiwa. Vilevile, malipo ya deni kama asilimia ya mapato ya serikali yamesimama kwenye asilimia 14.5, kiwango ambacho ni chini ya kikomo cha asilimia 18.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *