Benki ya CRDB imeingia makubaliano na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani (FAO) kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo kufanya kilimo bora kupitia teknolojia za kisasa.
Akizungumza katika halfa iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesisitiza utayari wa benki ya CRDB katika kuwawezesha wakulima kufanya kilimo cha kisasa kwa kuzingatia kuwa ndio benki pekee nchini yenye usaili wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya Tabianchi (UN GCF).
Ushirikiano huu wa CRDB na FAO pia unasaidia agenda ya Serikali ya 10/30 yenye lengo la kukuza sekta ya kilimo na kuifanya sekta hiyo kuingiza asilimia 10 ya ukuaji wa uchumi nchini ifikapo 2030.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa FAO kuingia makubaliano ya aina hii na taasisi za fedha barani Afrika. Benki ya CRDB inaongeza nchini kwa uwezeshaji wa sekta ya kilimo ikitoka asilimia 60 ya mikopo yote ya kilimo nchini.