Baada ya takribani miaka 12 ya kuikosa tuzo hiyo kwa kashfa mbalimbali hatimaye msanii Chris Brown ameshinda tuzo ya Grammy kwa mara nyingine tena.
Chris Brown amefanikiwa kushinda tuzo ya album bora ya Rnb “11:11 (Deluxe)” inayomfanya kufikisha jumla ya tuzo 2 za Grammy kwenye maisha yake ya muziki.Tuzo ya kwanza alipata mwaka 2012 kupitia album yake ya “F.A.M.E”.
Ushindi huu umekuwa ushindi wa mashabiki wa Chris Brown na tasnia ya muziki kwa ujumla ikiwa wengi huamini msanii huyo ni msanii bora kuwahi kutokea kwa kizazi chake.