Nyota wa muziki wa Rnb na Pop Chris Brown amewasilisha mashtaka dhidi ya Kampuni ya Filamu ya Warner Bros, Discovery akidai kampuni hiyo kiasi cha Tsh Trilioni 1.2 kwa madai ya kuchapisha taarifa za uongo zinazomdhalilisha kupitia Documentary ya “Chris Brown : A history of violence”.
Mwanasheria wa Chris Brown Levi McCathern amesema kuwa wameishtaki kampuni hiyo kulinda ukweli licha ya kwamba kampuni hiyo ilipewa ushahidi kuwa taarifa hizo sio za kweli bado kampuni hiyo iliandaa documentary hiyo na kuchapisha kwa makusudi.