Chelsea kikosi ghali zaidi barani Ulaya

Chelsea imetajwa kuwa kikosi cha gharama kubwa zaidi katika historia ya soka, kwa gharama ya uhamisho kufikia kiasi cha yuro bilioni 1.656(£1.39 bilioni), kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya UEFA. Hii inavunja rekodi zilizowekwa awali na Manchester United mwaka 2023 (€1.422 bilioni) na Real Madrid mwaka 2020 (€1.33 bilioni).

Tangu Todd Boehly na Clearlake Capital walipochukua klabu hiyo mwaka 2022, Chelsea imesajili wachezaji 41 katika dirisha sita za usajili, wakitumia karibu €2 bilioni katika uhamisho kati ya Julai 2019 na Juni 2024.

Hata hivyo, licha ya matumizi hayo makubwa, Chelsea ilimaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England katika nafasi ya sita na kwa sasa wanashika nafasi ya tano, ikionyesha kuwa mafanikio uwanjani hayajalingana na uwekezaji mkubwa walioufanya.

Usajili wa rekodi wa Chelsea ni Enzo Fernández, ambaye alijiunga kutoka Benfica mwaka 2023 akiwa mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina. Alitathminiwa kwa kiwango cha juu sana na kumfanya kuwa mchezaji wa tano ghali zaidi katika historia ya soka – na mchezaji ghali zaidi wa miaka ya 2020 – baada ya Chelsea kulipa £106.8 milioni kumpata.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *