Daniel Chapo wa Chama tawala cha FRELIMO ameapishwa kuwa Rais wa Msumbiji katika hafla iliyofanyika jijini Maputo.
Rais Chapo ameahidi kuzingatia umoja na kuongoza juhudi za maendeleo kote nchini.
Viongozi wa nchi mbalimbali walijumuika katika hafla hiyo akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa aliyemuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.