Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kuwa urafikia katia ya chama cha CCM na Prosperity Party ya nchini Ethiopia ni hatua muhimu ya kuboresha uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili.
Dkt Nchimbi ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za CCM kwenye Mkutano mkuu wa Prosperity Party uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini Ethiopia.
Dkt Nchimbi ameweka wazi kuwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Ethiopia umebebwa kwenye misingi imara ya itikadi za kisiasa iliyowekwa na waasisi wa nchi hizo mbili, huku akitoa wito kwa uongozi wa kizazi cha sasa unawajibika kuimarisha zaidi kwa ajili ya manufaa ya kiuchumi ya Wananchi wa pande zote.