BoT yahimiza wananchi kuacha kutumia Fedha za kigeni kununua bidhaa nchini.

Benki Kuu imewataka wananchi wote kutumia Shilingi ya Tanzania wakati wanapofanya miamala yao nchini katika nyanja mbalimbali.

Hayo yamezungumzwa na Gavana wa Benki Kuu Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba ambaye amesema ni kosa kununua, kuuza bidhaa na huduma hapa nchini kwa kutumia fedha za kigeni.

Ameongeza kuwa kutumia fedha za kigeni ni kuhujumu uchumi wetu na kunufaisha sera za fedha za nchi za kigeni.

Gavana amesema Benki Kuu itaendelea kusimamia utekelezaji wa kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu kinachohimiza matumizi ya Shilingi katika kufanya miamala hapa nchini ili kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni yasiyokimuwa na lazima.

Aidha Gavana Tutubi amesema kuwa hadi hivi sasa Benki Kuu imeshanunua tani 2.5 za dhahabu ikiwa ni jitihada za kuongeza akiba yetu ya fedha za kigeni huku lengo likiwa kununua tani 6 hadi kufikia mwisho wa mwaka wa mwaka huu wa fedha 2024/2025.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *