Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya African Export Import (AFREXIMBANK). Bw Haytham ElMaayergi ambapo wamejadili ambapo wamejadili kuhusu uwekezaji katika viwanda, kilimo na sekta ya madini na utalii.
Katika kikao hicho Gavana Tutubi amehimiza AFREXIMBANK kuwekeza zaidi katika sekta ya madini nchini hasa kwa kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati wa dhahabu.
Kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza upatikanaji wa dhahabu ambayo itanunuliwa na Benki Kuu na kuhifadhiwa kama sehemu ya akiba ya fedha za kigeni, hatua inayolenga kuimarisha uchumi wa taifa .