Arsenal imemteua Andrea Berta kama Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa klabu hiyo kuelekea msimu ujao. Berta anajiunga na Arsenal akitokea Atletico Madrid ambapo alifanya kazi kwa muda mrefu na kwa mafanikio.
Katika kipindi chake Atletico Berta alifanikiwa kuwezesha usajili wa nyota kama Antoine Griezman, Luis Suarez, Julian Alvarez, Joao Felix, Angel Correa Rodrigo De Paul na wengine kibao, usajili ambao uliwapa mafanikio Atletico ikiwemo kubeba ubingwa wa La Liga mara 2 pamoja na makombe ya Europa league na Super Cup.
Berta anakuja kufanya kazi na Mikel Arteta kwenye kuendelea kukijenga kikosi cha Arsenal akichukua nafasi ya Edu Gaspar ambaye aliachia ngazi mwaka jana mwishoni akitimkia Nottingham Forest.