Mchezo wa fainali ya Super Cup iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu baina ya Barcelona dhidi ya Real Madrid unaojulikana zaidi kama El Classico umemalizika kwa ushindi mnono wa Barcelona wa mabao 5-2 dhidi ya hasimu wake mkubwa Real Madrid.
Kombe hili linakuwa la kwanza kwa kocha Hans Flick akiwa na msimu wake wa kwanza ndani ya Barcelona. Mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua ulimalizika kwa Barcelona kushinda taji hilo mbele ya hasimu wake Real Madrid.
Ushindi huo kwa Barcelona unakuwa wa pili msimu huu dhidi ya Real Madrid baada ya ule wa mabao 4-0 ugenini Santiago Bernabeu katika mzunguko wa kwanza wa ligi ya La Liga.
Wawili hao wanatarajiwa kukutana tena kwenye ligi ambapo Barcelona atamkaribisha Real Madrid katika dimba la Nou Camp ikiwa mchezo utakaovuta hisia za wengi kwani wawili hao wanagombania ubingwa wa ligi kuu nchini Uhispania.