Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Watumishi wote wa taasisi hiyo wametakiwa kila mmoja wao kutimiza wajibu wake katika nafasi yake kwa weledi, ubunifu, uaminifu na ufanisi ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo yamebainishwa leo Februari 21, 2025 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Morena Mkoani Morogoro.
Amesema, baraza la Wafanyakazi ni chombo pekee kinachoweza kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi ambalo lipo kwa mujibu wa Agizo la Rais Na. 1 la Mwaka 1970 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa ngazi zote.
“Naelewa kuwa Taasisi inatekeleza majukumu muhimu sana ya kutoa huduma za za tafiti za jiosayansi Jiolojia na Utafiti wa Madini kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini na wananchi kwa lengo la kubaini aina za miamba na madini inayopatikana nchini. Aidha, taasisi hii mdau mkubwa katika kufikia lengo la maono ya 2030 (Vision 2030). Hivyo kupitia baraza hili viongozi wanatakiwa kupata mawazo mapya ya kuboresha utendaji kazi amesema Mbibo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa GST ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Mbibo kwa kushiriki na kulifungua Baraza hilo ambapo ameahidi kuyatekeleza yale yote yaliyoelekezwa na mgeni rasmi na pia amewataka Wajumbe wa Baraza hilo kutoa maoni na michango yao kwa uhuru na uwazi ili kuboresha utendaji kazi