Baraza la Maaskofu latahadharisha matumizi ya Akili Unde

Baraza la Maaskofu Tanzania limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha kunakuwa na mwongozo madhubuti kuhusu matumizi na ulinzi wa akili unde au akili mnemba au bandia kama wengine wanavyoita (Artificial Intelligence -Al) kuelekea mwaka 2050, ili kulinda taifa dhidi ya hatari zinazoweza kuibuka kutokana na matumizi ya teknolojia hiyo katika miaka 25 ijayo.

Akizungumza leo Jumatatu, Januari 13, 2024, wakati wa mkutano wa viongozi wa Taasisi za Kidini Jijini Dar es Salaam kuhusu rasimu ya kwanza ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, Mariana Balampama, Mjumbe Mshauri wa baraza hilo, ametaja hatari zinazoweza kuletwa na matumizi makubwa ya akili unde kuwa ni pamoja na wingi wa taarifa potofu, kuvuja kwa taarifa binafsi, na masuala ya ulinzi na usalama wa taifa.

Akili unde (Al) ni teknolojia inayotumika kuunda mifumo ya kompyuta yenye uwezo wa kufanya kazi zinazohitaji akili ya binadamu, kama vile kuona, kutambua sauti, kufanya maamuzi na kutafsiri lugha. Teknolojia hii inatumika katika viwanda, serikalini, na tafiti za kisayansi, na ina matumizi katika injini za utafutaji, mifumo ya mapendekezo, utambuzi wa sauti, magari yanayojiendesha, roboti za mazungumzo, uzalishaji picha, na michezo ya kimkakati.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *