Aziz Ki afunga ndoa na Hamisa Mobetto.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephan Aziz Ki rasmi amefunga pingu za maisha na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Wawili hao wamefungishwa ndoa na jopo la masheikh likiongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar katika msikiti wa Masjid Nnuur uliopo Mbweni, Dar es Salaam.

Hamisa alilipiw mahari ya ng’ombe 30 na milioni 30 na Aziz Ki, mahari iliyokabidhiwa na Rais wa klabu ya Yanga Hersi Said kwa niaba ya familia ya Bwana harusi.

Akizungumza baada ya kufungisha ndoa hiyo Sheikh Walid amewatakia heri wanandoa hao huku akisisitiza watu kuepuka zinaa. Baada ya ndoa hiyo kufungwa sherehe zilifata kufanyika Superdome Masaki jijini Dar es Salaam.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *