Al Jazeera yafungiwa kurusha matangazo DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekifungia kituo cha televisheni cha Al Jazeera kutokana na kudaiwa kurusha mahojiano na kiongozi wa kundi la Waasi wa M23, Bertrand Bisimwa.

Haya yamezungumzwa na Msemaji wa Serikali ya DRC, Patrick Muyaya kupitia Shirika la Habari la DW akielezea kuwa mamlaka zimebatilisha kibali cha kurusha matangazo cha televisheni hiyo.

Muyaya amesema Al Jazeera walirusha mahojiano hayo bila kupata kibali maalumu ambapo kwenye mahojiano hayo Bisimwa aliishutumu Serikali ya DRC kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya Agosti.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria wa DRC, Constant Mutamba amesema waandishi wa habari au mtu yeyote atakayeripoti kuhusu shughuli za jeshi la Rwanda na waasi wa M23, atashtakiwa.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *