Al Ahly yagomea mchezo wa dabi.

Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imegoma kushiriki mchezo wao wa dabi dhidi ya Zamalek kwa kile kinachodaiwa kuwa ukiukwaji wa makubaliano uliofanywa baina ya timu hizo na shirikisho la soka la Misiri (EFA).

Taarifa zinadai kuwa makubaliano yalikuwa kuteua mwamuzi wa kigeni badala ya kutumia waamuzi wa ndani kwenye mchezo baina ya timu hizo 2, jambo ambalo limeshindikana kwa mchezo wa leo na kutafsiriwa kama kinyume na makubaliano na Al Ahly.

Mbali na kugomea mchezo huo wa leo Al Ahly wametishia kujitoa ligi hiyo endapo makubaliano hayo hayatatekelezwa. Mchezo huo wa dabi ulikuwa ni moja ya michezo ya kuamua bingwa wa ligi hiyo msimu huu ambapo timu tatu za ligi hiyo zinapambania.

Aidha EFA bado hawajatoa tamko lolote kuhusiana na sintofahamu hiyo ya mgomo wa Al Ahly kuelekea mchezo huo wa dabi licha ya awali shirikisho kudai muda haukutosha kupata waamuzi wa nje na kuwataka Al Ahly kuunga mkono waamuzi wa ndani, jambo ambalo limekuwa gumu kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Misiri.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *