Ajali ya ndege Philadelphia yaua 6 wakiwemo wagonjwa wawili.

Ajali ya ndege yatokea katika mji wa Philadelphia nchini Marekani ambapo ndege hiyo inaripotiwa kuanguka katika barabara karibu na jumba la maduka ya Rossevelt, hali iliyosababisha magari na nyumba zilizokuwa jirani kushika moto.

Ndege hiyo inasemekana ilikuwa na watu 6 ambapo wawili wanadaiwa kuwa ni wagonjwa raia wa Mexico pamoja na wahudumua wanne , aidha mashuhuda wamedai waliona moshi mzito ukitanda eneo la ajali.

Hadi sasa idadi ya waliofariki na majeruhi haijathibitishwa vizuri bado licha ya baadhi ya majeruhi kukimbizwa hospitalini kwaajili ya matibabu.

Vikosi vya uokojai vilifika na kujaribu kupambana na moto uliosambaa kwenye nyumba kadhaa kutokana na ajali hiyo karibu na mtaa wa 2900 wa Cottman Avenue.

Mshirikishe Mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *