Shirika la habari la Associated Press limethibitisha kuwa ajali ya ndege mbili ndogo kusini mwa jimbo la Arizona nchini Marekani imesababisha vifo vya watu wawili.
Ajali hiyo inayosemekana kutokea uwanja wa ndege wa Marana Tucson ilihusisha ndege mbili ambapo kila ndege ilikuwa na abiria wawili, taarifa zinadai baada ya mgongano huo ndege moja iliweza kutua salama huku nyingine ikianguka karibia na njia ya kurukia kisha kuwaka moto.
Aidha Idara ya polisi imethibitisha vifo vya watu wawili kwenye ajali hiyo, huku uchunguzi ukiendelea kwa taarifa zaidi.