Baada ya kuvunja mkataba na Rapa Kanye West mwishoni mwa 2022, Kampuni ya Adidas imeripotiwa kuuza bidhaa zake zote zilizosalia za viatu vya Kanye West aina ya “Yeezy” vyenye thamani ya Tsh, Trilioni 1.2 rasmi ikihitimisha uhusiano wao na rapa huyo.
“Hakuna hata jozi moja ya viatu vya Yeezy iliyobaki, vyote vimeuzwa na ukurasa huo tayari tumeufunga” alisema Mkuu wa Fedha wa Adidas Bw. Harm Ohlmeyer.
Ikumbukwe uhusiano baina ya kampuni hiyo na rapa huyo ulififia baada ya kauli za chuki alizotoa rapa huyo mwaka 2022 dhidi ya wayahudi jambo ambalo liliwakasirisha Adidas na kuwafanya kuuza sehemu ya hisa za Yeezy na kutoa mapato kwa mashirika yenye hisani yanayopinga ubaguzi dhidi ya wayahudi jambo ambalo lilizua mzozo uliopelekea kufikishana mahakamani baina ya pande hizo mbili.