Kamati ya uongozi taifa ya chama cha ACT wazalendo imesema haitashiriki vikao vya baraza la vyama vya siasa ikidai sababu tatu za kufikia uamuzi huo ni kutokana na vikao hivyo kugeuka jukwaa la kuhalalisha na kusafisha uchafuzi na wizi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024.
Aidha wamedai kuwa baraza hilo linaloratibiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kupoteza uhalali baada ya kushindwa kuwa jukwaa la majadiliano kati ya Serikali na vyama vya siasa kwaajili ya kujenga na kukuza misingi ya demokrasia ya vyama vingi.
Sababu ya tatu wamedai Serikali kupuuza maazimio ya baraza hilo ya kuboresha uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika Oktoba 11, 2024 Dodoma na kutanguliwa na vikao vya kamati za baraza na kamati ya uongozi wa baraza.