Beki wa timu ya taifa ya Morocco па klabu ya Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi, hatacheza katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania kutokana na kufungiwa baada ya kuoneshwa kadi mbili za njano katika mechi zilizopita dhidi ya Niger na Tanzania.
Mechi hiyo ni sehemu ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo Morocco inaongoza Kundi E na inalenga kufuzu kwenye michuano hiyo ya timu 48 itakayofanyika nchini Marekani, Canada, na Mexico.
Hakimi, anayejulikana kama mmoja wa mabeki bora duniani, ni nahodha wa Morocco na amekuwa akiongoza timu hiyo kwenye mashindano makubwa kama Kombe la Dunia la FIFA na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).